.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 26 Novemba 2015

Tagged Under:

Didier Drogba anarudi Chelsea kama kocha? majibu yake haya hapa

By: Unknown On: Alhamisi, Novemba 26, 2015
  • Share The Gag

  • Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba amesema matarajio yake ya sasa ni kuona anarudi kwenye klabu yake ya zamani ya Chelsea kama kocha.
    Drogba, ambaye kwa sasa anacheza soka ya kulipwa ya Montreal Impact huko Canada, aliifungia Chelsea jumla ya mabao 164 wakati akiitumikia klabu hiyo.
    Mshambuliaji huyo amesema angependa kuihudumia klabu hiyo baada ya kukamilika kwa kipindi chake cha  uchezaji.
    ”Tayari nimekubaliana na wakurugenzi wa klabu hiyo kuwa ninaweza kurejea kuwa meneja kwa sababu klabu hiyo ilinisaidia sana, pia imenikuza katika kipaji changu cha mpira”..
    Drogba ndiye aliyeifungia Chelsea bao lililoipa ushindi na taji la mabingwa wa bara Ulaya mwaka wa 2012 pia aliisaidia Chelsea kunyakuwa mataji 4 ya ligi kuu ya Uingereza kabla ya kuhamia Canada kujiunga na klabu ya Montreal Impact.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni