.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatano, 25 Novemba 2015

Tagged Under:

Kipigo kilichowakuta AS Roma vs FC Barcelona bora ya Real Madrid, Full Time za UEFA Nov 24

By: Unknown On: Jumatano, Novemba 25, 2015
  • Share The Gag


  • Mshikemshike wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi imeendelea tena usiku wa November 24 katika viwanja mbalimbali barani Ulaya, usiku wa November 24 zimechezwa jumla ya mechi nane zinazohusisha timu kutoka Kundi E, F, G na H, miongoni mwa mechi zilizochezwa na kushuhudia idadi kubwa ya magoli ni mechi kati ya FC Barcelona dhidi ya Roma.
    Huu ukiwa ndio mchezo wa pili wa Lionel Messi toka arejee dimbani baada ya kuuguza jeraha la goti kwa zaidi ya wiki tatu, Roma ambao walikuwa ugenini katika dimba la Nou Camp jijini Barcelona walipata bahati mbaya kurejea kwa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina, kwani alionekana kama mtu ambaye hajatoka majeruhi kutokana na kuendelea kucheza katika kiwango bora.
    2EC7879D00000578-0-image-a-17_1448397858137
    FC Barcelona walifanikiwa kuiadhibu Roma kwa jumla ya goli 6-1 magoli ambayo yalifungwa katika mfumo ule ule wa FC Barcelona uliyozoeleka wa pasi fupi fupi lakini zenye madhara kwa Roma. Ilichukua dakika 15 za mwanzo tu FC Barcelona kupata goli la kwanza baada ya Luis Surez kuitumia vyema pasi kutoka kwa Dani Alves.
    2EC783E400000578-0-image-a-20_1448397862932
    Goli la pili la FC Barcelona lilifungwa na Lionel Messi dakika ya 18 ya mchezo kabla ya Luis Suarez kufunga goli la tatu dakika ya 44, goli la nne lilifungwa na Gerrard Pique dakika ya 56, Lionel Messi dakika ya 60 kabla ya Adriano kupachika goli la sita dakika ya 77, Roma ambao walikuwa hawaamini kilichowakuta walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi kutoka kwa Edin Dzeko dakika ya 90.
    Matokeo ya mechi nyingine za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizochezwa November 24
    KUNDI E
    • BATE Borisov 1 – 1 Bayer Leverkusen
    • FC Barcelona 6 – 1 Roma
    KUNDI F
    • Arsenal 3 – 0 Dinamo Zagreb
    • Bayern Munich 4 – 0 Olympiakos
    KUNDI G
    • FC Porto 0 – 2 Dynamo Kyiv
    • Maccabi Tel Aviv 0 – 4 Chelsea
    KUNDI H
    • Zenit St. Petersburg 2 – 0 Valencia
    • Lyon 1 – 2 Gent

    0 maoni:

    Chapisha Maoni