.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 5 Novemba 2015

Tagged Under:

Full Time ya Rubin Kazan Vs Liverpool na matokeo ya mechi nyingine za Europa Ligi November 5

By: Unknown On: Alhamisi, Novemba 05, 2015
  • Share The Gag

  • Usiku wa November 4 kulichezwa michezo kadhaa ya mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya na tuliona baadhi ya vilabu vikiondoka na point tatu kwa furaha na timu nyingine zikiondoka vichwa chini baada ya kupoteza michezo hiyo, Usiku wa November 5 mechi za UEFA ndogo zilipigwa kama kawaida.
    2198682_heroa
    Klabu ya Liverpool ya Uingereza ililazimika kusafiri hadi Urusi kucheza na Rubin Kazan katika muendelezo wa mechi za Kundi B, Liverpool wakiwa ugenini wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, licha ya kuwa walikuwa ugenini Liverpool walifanikiwa kuibuka na point tatu mbele ya Rubin Kazan.
    3000
    Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika hakuna timu iliyokuwa imefanikiwa kuona lango la mpinzani wake, kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kucheza kwa tahadhari, kabla ya dakika ya 52 Liverpool walifanikiwa kupata goli la kwanza kupitia kwa Jordon Ibe, goli ambalo lilidumu kwa dakika zote 90.
    3000 (1)
    Baadhi ya Matokeo ya mechi nyingine za UEFA EUROPA LEAGU November 5
    • Ajax 0 – 0 Fenerbahce
    • Celtic 1 – 2 Molde
    • Sion 1 – 1 Bordeaux
    • Borussia Dortmund 4 – 0 FK Qabala
    • FC Krasnodar 2 – 1 PAOK Thessaloniki FC
    • Club Brugge 1 – 0 Legia Warszawa
    • SSC Napoli 5 – 0 FC Midtjylland
    • Dinamo Minsk 1 – 2 Villarreal
    • Viktoria Plzen 1 – 2 Rapid Wien
    Magoli ya Rubin Kazan Vs Liverpool

    0 maoni:

    Chapisha Maoni