.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 24 Novemba 2015

Tagged Under:

Achana na stori za Mwasika wa Yanga kumpiga refa, kutana na video ya kituko cha refa anakupiga na kadi anakupa…

By: Unknown On: Jumanne, Novemba 24, 2015
  • Share The Gag

  • Mchezo wa soka ni mchezo ambao unapendwa na watu wengi duniani ila mtu pekee ambaye anatajwa kuwa na nafasi ya kuweza kufanya maamuzi ndani ya uwanja ni refa ambaye mara nyingi amekuwa akiambulia lawama kutoka kwa wachezaji na viongozi wa timu wanaoamini kuwa wameonewa, najua umewahi kusikia refa akipigwa na wachezaji au mashabiki wa timu fulani.
    maxresdefault (1)
    Hata kuna wakati wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Stephane Mwasika waliwahi kumpiga refa Israel Nkongo ambaye waliamini kuwa hakuchezesha mechi yao kwa haki bali alipendelea Azam FC, tukio ambalo liliwafanya wapate adhabu, achana na beki huyo wa Yanga wa zamani mtu wangu, nimekutana na video mtandaoni ya vioja vya refa mbabe.
    01
    Wachezaji wa Yanga wakimkimbiza refa wa mechi yao dhidi ya Azam FC  Israel Nkongo
    Najua umezoea kusikia wachezaji wakimpiga refa, ila refa huyu anakupiga na kadi anakuonesha kama unapingana na uamuzi wake, cheki kipande cha video cha dakika 2 baada ya refa kuamuru penati wachezaji walianza kumzonga na yeye akawa anawakwepa ila baadae akampiga ngumi mchezaji hadi na kumuangusha chini na mwingine alimpiga teke yaani hataki kukupa nafasi ya kumpiga.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni