.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumapili, 6 Septemba 2015

Tagged Under:

HII NDIYO MILIMA NA MABONDE YA KUVUKA TAIFA STARS KUELEKEA GABON 2017

By: Unknown On: Jumapili, Septemba 06, 2015
  • Share The Gag


  • Baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars kutoka kulia Farid Mussa, Mrisho Ngassa, Mwinyi Hajji Mngwali, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta

    MATOKEO NA RATIBA YA MECHI ZA KUNDI G

    Jumamosi Juni 13, 2015 Nigeria 2-0 Chad Misri 3-0 Tanzania Jumamosi Sept 5, 2015 Tanzania 0-0 Nigeria Jumapili Sept 6, 2015 Chad v Misri Ijumaa Machi 25, 2016 Chad v Tanzania Nigeria v Misri Jumatatu Machi 28, 2016 Tanzania v Chad Misri v Nigeria Jumamosi Juni 4, 2016 Chad v Nigeria Tanzania v Misri Jumamosi Sept 3, 2016 Nigeria v Tanzania Misri v Chad
    TANZANIA itahitimisha mechi za mzunguko wa kwanza wa Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 Machi mwakani, itakapoifuata Chad.
    Taifa Stars Jumamosi imejiweka njia panda katika mbio za AFCON 2017, baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Nigeria, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Taifa Stars sasa inakamilisha mechi mbili za Kundi G bila ushindi, baada ya awali kufungwa mabao 3-0 na Misri mjini Alexandria Juni mwaka huu, wakati Nigeria inafikisha pointi nne baada ya awali kushinda 2-0 dhidi ya Chad.
    Misri watakuwa wageni wa Chad Jumapili kukamilisha raundi ya pili ya Kundi G. Wote Tanzania na Nigeria wataiombea mabaya Misri Jumapili ifungwe ili isipae zaidi katika kundi hilo.
    Lakini Misri wanapewa nafasi kubwa ya kushinda na matokeo mabaya sana kwao yanaweza kuwa sare, kwani Chad si timu ya kubeza sana.
    Tanzania bado ina nafasi japo finyu ya kwenda Gabon mwaka 2017, iwapo itashinda mechi zake zilizobakia kuanzia ya Machi 25 mwakani dhidi ya Chad.

    MSIMAMO WA KUNDI G

    NaTimuPWDLGFGAGDPts
    1Nigeria21102024
    2Misri11003033
    3Tanzania201103-31
    4Chad100102-20

    0 maoni:

    Chapisha Maoni