.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 25 Agosti 2015

Tagged Under:

TETESI ZA UHAMISHO: NEYMAR KWENDA MAN UNITED!

By: Unknown On: Jumanne, Agosti 25, 2015
  • Share The Gag


  • Manchester United wameripotiwa kutoa Ofa inayokaribia Pauni Milioni 140 kumnunua Straika wa Barcelona ambae ni Kepteni wa Brazil, Neymar, kwa mujibu wa Chombo cha Habari cha huko Brazil Globo Esporte.
    Inaaminika Mkataba wa Barcelona na Neymar, mwenye Miaka 23, una kipengele kinachotaka Mabingwa hao wa Spain walipwe Dau la Pauni Milioni 140 ikiwa atataka kuhama kabla Mkataba kumalizika.

    Globo Esporte ndicho Chombo cha Habari cha kwanza kutoboa Mwezi uliopita kwamba Mbrazil Roberto Firmino yupo njiani kujiunga na Liverpool na kitu hicho kikatokea kweli.
    Habari hizo kutoka Brazil pia zimedai Neymar yeye hana kipingamizi chochote cha kucheza England na hasa Man United ambayo anaiona ni Klabu kubwa Duniani na yenye historia iliyotukuka.

    Hapo Jana, mara baada ya Barcelona kuifunga Athletic Bilbao Bao 1-0 katika Mechi yao ya kwanza kabisa ya La Liga katika Msimu huu mpya, Kocha wao Luis Enrique alikataa kuongea lolote kuhusu uvumi huu.
    Hiyo Jana Neymar hakucheza Mechi hiyo kwani alikuwa mgonjwa na alianza tena mazoezi hivi Juzi tu.
    Mapema kwenye Dirisha la Uhamisho hili, Meneja wa Man United Louis van Gaal aliwahi kudokeza wao wanaweza kuleta maajabu katika Soko la Uhamisho.
    Mwezi Julai, wakiwa Ziarani huko USA, Van Gaal aliwahi kusema kuhusu Straika ambae watamnunua: “Si Straika ambae Vyombo vya Habari vinamzunguzia. Itabidi mkae na kusubiri.”

    0 maoni:

    Chapisha Maoni