Ninayo Good News imenifikia mtu wangu ambayo Watanzania wengi na wakazi wa Dar es salaam tulikua tukiisubiri kwa muda mrefu ni kuhusu kukamilika kwa mradi wa Mabasi yaendayo haraka ambayo zaidi ya mwaka na nusu yaliingia kwenye headlines za kuwa yatatoa huduma hizo.
Habari ikufikie kuwa Mabasi hayo rasmi yanaanza kazi August 17 Jumatatu kuanzia saa 3 asubuhi nje ya kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo
ambako kutafanyika uzinduzi wa kuanza huduma ya mpito kisha Wananchi
wataruhusiwa kupanda mabasi hayo kutoka Ubungo kwenda Kimara na kutoka
Kimara hadi Kivukoni Bure.
Kwa bara la Afrika,jiji la Dar es salaam litakua la pili kutekeleza
mradi huu mtu wangu baada ya Afrika Kusini na litakua jiji la kwanza kwa
nchi za Afrika Mashariki,Kaskazini na Kati.
DeusiDedith Mutasingwa ambaye ni
Afisa wa masuala ya fidia katika mradi wa mabasi haya yaendayo haraka
yaliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za
mitaa,amesema yapo mabasi ya aina mbili kuna yale ya mita 18 ambayo yana uwezo wa kubeba abiria 140 na yapo yenye uwezo wa kubeba watu 80.
Amesema mabasi hayo pia yamezingatia watu wenye mahitaji maalum kama Walemavu na Wajawazito,pia
Wafanyabiashara wanaopanga vitu vyao pembeni ya Barabara na kwenye
vituo wameombwa kuviondoa na kwa wale watakaonekana kukaidi amri hiyo
faini yake si chini 250,000.
Jumapili, 16 Agosti 2015
Tagged Under:
Mabasi yaendayo haraka inatengenezwa Aug 17 Dsm na safari zake
By:
Unknown
On: Jumapili, Agosti 16, 2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni