Sergio Aguero akishangilia bao lake la kwanza dhidi ya Chelsea.Mbele ya Mashabiki 54,331 Uwanjani kwao Etihad, Manchester City Leo wamewabonda Mabingwa wa England Chelsea Bao 3-0 katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Wakati huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa City wa 3-0 kila Mechi tangu Ligi ianze Wikiendi iliyopita, kwa Chelsea hii ni Mechi yao ya pili bila ushindi baada kuanza kwa Sare ya 2-2 huko kwao Stamford Bridge walipocheza na Swansea City.
Hii
Leo City walistahili ushindi dhidi ya Chelsea ambayo kwenye Benchi lake
Leo alikosekana Daktari wao Mwanamama maarufu Eva Carneiro ambae
amepigwa marufuku na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho baada kutofautiana.
Ramires kati
Matic na Silva wakibanan
Baada
ya Man City kupiga hodi mara kadhaa huku wakisimamishwa na ushujaa wa
Kipa wa Chelsea Asmir Begovic ambae alikuwa Golini kuchukuwa nafasi ya
Kipa Nambari Wani Thibaut Courtois aliefungiwa Mechi 1 baada ya Kadi
Nyekundu katika Mechi iliyopita waliyotoka 2-2 na Swansea City, Man City
walifanikiwa kufunga katika Dakika ya 31.
Kweupeee 1-0
1-0
Bao hilo lilitokana na pasi safi ya David Silva na kumkuta Sergio Aguero alieachia shuti la chini na kutinga. Kipindi cha Pili kilianza kwa Chelsea kufanya kitu cha ajabu kwa kumpiga Benchi Nahodha wao John Terry na kumuingiza Kurt Zouma nah ii ni mara ya kwanza kwa Jose Mourinho kuwahi kumpumzisha Nahodha wake kwa staili hiyo.
Kepteni
wa Man City, Vincent Kompany aliipa Timu yake Bao la Pili katika Dakika
ya 79 kwa kichwa baada ya kuunganisha Kona ya David Silva.
Akipata matibabu kutoka kwa daktari wa timu
Diego Costa
Diego Costa chini!Dakika ya 84, City wakawa 3-0 mbele kwa Bao la Fernandinho aliefunga kwa shuti kutoka nje tu ya boksi.
Vincent Kompany dakika ya 79 na Fernandinho dakika ya 85
Hatari tupu!! 1-0
Sergio Agüero dakika ya 31aliipatia bao la kuongoza na mtanange kwenda mapumziko ukiwa 1-0 dhidi ya Chelsea.
2-0 Kompany akiwachoma bao Chelsea
Vicent Kompany akishangilia bao lake la pili
Bao la pili kwa Kompany msimu huu mpya Ligi Kuu England
3-0

0 maoni:
Chapisha Maoni