.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumapili, 30 Agosti 2015

Tagged Under:

STARS SASA KUPIGA MAZOEZI MARA MOJA TU KWA SIKU HAPA UTURUKI

By: Unknown On: Jumapili, Agosti 30, 2015
  • Share The Gag


  • Na Saleh Ally, Kartepe
    Kikosi cha Taifa Stars sasa kitaendelea na mazoezi mara moja tu kwa siku kwa siku zote zilizobaki za kambi yake hapa nchini Uturuki.


    Stars imeweka kambi ya siku nane hapa Kartepe, Uturuki kujiandaa na mechi yake dhidi ya Nigeria itakayopigwa Septemba 5 jijini Dar es Salaam.

    Kocha Mkuu wa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema watakuwa wakifanya mazoezi mara moja kwa siku wakiwa wamelenga zaidi masuala ya ufundi.

    “Sasa tunaangalia ufundi zaidi huku kidogokidogo tunatunza fitness. Pia hatuwezi kufanya mazoezi makali sana kama ilivyokuwa mwanzo kwa kuwa tunakwenda kwenye mechi,” alisema Mkwasa.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni