.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 13 Agosti 2015

Tagged Under:

ASTON VILLA vs MANCHESTER UNITED LEO

By: Unknown On: Alhamisi, Agosti 13, 2015
  • Share The Gag

  • Kwa sababu za kiusalama Gemu ya Ligi Kuu England kati ya Aston Villa na Manchester United imewekwa Ijumaa Usiku kutokana na Mji wa Birmingham kuwa na Maandamano badala ya kuchezwa Wikiendi.
    Mechi hii, ambayo itachezwa Villa Park, inazikutanisha Timu ambazo zilishinda Mechi zao za kwanza za Msimu mpya Wikiendi iliyopita kwa zote kushinda kwa Bao 1-0.
    Man United walishinda kwao Old Trafford kwa kuiangusha Tottenham kwa Bao la kujifunga mwenyewe Beki wa Tottenham Kyle Walker wakati Villa wakishinda Ugenini walipocheza na Timu mpya kabisa kwenye Ligi Kuu England Bournemouth huku Bao lao moja likifungwa na Rudy Gestede.
    Kila Timu itatinga kwenye Mechi hii ikiwakosa baadhi ya Wachezaji wake kwa Man United kuwakosa Marouane Fellaini, ambae yuko Kifungoni na hii ni Mechi yake ya pili akibakiza moja, na pia watamkosa Majeruhi Phil Jones.
    Villa wao wana Majeruhi Gary Gardner, Jores Okore na Jack Grealish na wote wana hati hati kucheza Mechi hii.

    Mchezo huo utapigwa kesho ijumaa 14th Aug, 2015 kwenye Uwanja wa nyumbani wa Villa Park, Birmingham.

    USO KWA USO
    22.04.13 PRE Manchester United Aston Villa 3 : 0
    04.04.15 PRE Manchester United Aston Villa 3 : 1
    20.12.14 PRE Aston Villa Manchester United 1 : 1
    29.03.14 PRE Manchester United Aston Villa 4 : 1
    15.12.13 PRE Aston Villa Manchester United 0 : 3


    VIKOSI VINATEGEMEA KUWA HIVI:
    Man United (4-3-3): Romero, Darmian, Smalling, Blind, Shaw, Schneiderlin, Carrick, Mata, Depay, Young, Rooney.

    Aston Villa (4-2-3-1): Guzan, Bacuna, Richards, Clark, Amavi, Gueye, Westwood, Sanchez, Ayew, Sinclair, Gestede.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni