Tagged Under:
KOCHA ENRIQUE AMWAMBIA PEDRO SAFARI YAKE KWENDA MAN UNITED NI YEYE MWENYEWE SASA!
By:
Unknown
On: Alhamisi, Agosti 13, 2015
Kukiwa
na kila dalili kuwa Fowadi wa Barcelona Pedro yuko njiani kwenda
Manchester United, Kocha wa Mabingwa hao wa Spain Luis Enrique
amesisitiza ni juu ya Mchezaji huyo mwenyewe kuamua nini hatima yake.
Pedro,
mwenye Miaka 28, aliijulisha rasmi Barcelona Juzi Jumanne nia yake
kuhama ikiwa ni Masaa kadha kabla hajaifungia Klabu hiyo Bao la ushindi
walipotwaa UEFA Super Cup kwa kuibwaga Sevilla 5-4.
Akiongea
na Waandishi wa Habari, Luis Enrique alisema: “Tumesikia maoni yake, ni
uamuzi mgumu anaotakiwa kufanya lakini tutasubiri tujue ataamua nini.
Yeye anataka kuhama kwa vile hapati namba lakini tunataka acheze na ni
uamuzi mgumu.”
Hata hivyo, Enrique amesema Pedro ataanza Mechi ya
Kwanza ya Supercopa de Espana hapo Ijumaa huko Estadio San Mames, Bilbao
watakapocheza na Athletic Bilbao.
0 maoni:
Chapisha Maoni