.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatano, 12 Agosti 2015

Tagged Under:

TRA 'WAVAMIA' SIMBA NA YANGA SC, WOTE NA AZAM FC, MBEYA CITY...

By: Unknown On: Jumatano, Agosti 12, 2015
  • Share The Gag
  • MAMLAKA ya Kodi na Mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kuendesha semina ya kodi kwa viongozi wa vilabu viliyopo jijini Dar es salaam, siku ya ijumaa tarehe 14 Agosti katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la Kisutu.
    TRA itaendesha semina hiyo kwa vilabu vilivyopo ligi kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili ambapo viongozi wakuu wa vilabu hivyo, Katibu Mkuu, Mwenyekiti, na Mhasibu wanapaswa kuhudhuria semina hiyo.
    Kwa kuanzia TRA itaendesha semina hiyo jijini Dar es salaa, na baadae kuendelea na semina hizo kwa vilabu vilivyopo mikoani kwa lengo la viongozi wa vilabu kutambua umuhimu wa ulipaji kodi kwa wachezaji, makocha wanaowaajiri katika vilabu vyao.

    Semina hiyo itaanza saa 3 asubuhi mpaka saa 5 kamili asubuhi katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la Kisutu jijini Dar es salaam, vionggozi wa vilabu vya ligi kuu, ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili waliopo jijini Dar es salaam mnaombwa kuhudhuria semina hiyo.
    Timu zinazoshiriki Ligi Kuu ni Majimaji ya Ruvuma, Mbeya City, Prisons za Mbeya, Azam FC, Simba SC, Yanga SC za Dar es Salaam, Ndanda ya Mtwara, JKT Ruvu ya Pwani, Mtibwa Sugar ya Morogoro, Mgambo JKT, African Sports, Coastal Union za Tanga, Mwadui, Stand United za Shinyanga, Toto Africans ya Mwanza na Kagera Sugar ya Bukoba. 
    Wakati huo huo: Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Adam Mambi kwa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini.Katika Salam zake kwa Jaji Mambi, Malinzi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Kikwete kwa kumteua mwanafamilia huyo wa mpira wa miguu nchini kushika wadhifa huo.
    TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu na watanzania wote inamtakia kila la kheri Jaji Adam Mambi katika majukumu yake mapya ya Ujaji katika Mahakama Kuu nchini Tanzania.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni