

West Brom, chini ya Meneja Tony Pulis, huenda wakamkosa Beki wao ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man City, Joleon Lescott, ambae ana maumivu lakini Wachezaji wao wapya, Rickie Lambert, James McClean na James Chester wapo tayari kucheza isipokuwa Serge Gnabry kutoka Arsenal ambae Uhamisho wake haukukamilika kwa wakati.
Manchester City, chini ya Meneja Manuel Pellegrini, itawakosa Gael Clichy na Fabian Delph wote wakiwa na maumivu lakini David Silva, Samir Nasri na Sergio Aguero, ambao walikuwa wagonjwa, wako fiti kuanza Mechi hii.

-Manchester City hawajafungwa na WBA katika Mechi zao 5 zilizopita Uwanjani The Hawthorns, wakishinda 4 kati ya hizo.
-City, wakicheza kwao Etihad na hapo The Hawthorns, wameifunga WBA mara 7 mfululizo.

Referee: Mike Dean Assistants: S Long, M Perry Fourth Official: M Clattenburg

LIGI KUU ENGLAND
Jumatatu Agosti 10
22:00 West Brom v Man City
Ijumaa Agosti 14
22:45 Aston Villa v Man United
Jumamosi Agosti 15
14:45 Southampton v Everton
17:00 Sunderland v Norwich
17:00 Swansea v Newcastle
17:00 Tottenham v Stoke
17:00 Watford v West Brom
17:00 West Ham v Leicester
0 maoni:
Chapisha Maoni