Mchezaji
 wa Manchester United Memphis Depay amekwaruzana na Mchezaji wa zamani 
wa Klabu hiyo Robin van Persie wakati wa mazoezi wa Timu ya Taifa ya 
Netherlands. Tukio hilo limethibitishwa na Kocha wa Netherlands Danny 
Blind lakini amepuuza umuhimu wake na imefahamika kuwa lilitokea kabla 
ya Mechi ya Jumamosi ya EURO 2016 ambayo Netherlands iliifunga 
Kazakhstan 2-1. 
Kocha
 Blind, ambae mwanawe, Daley, ni Mchezaji mwenzake Depay huko Man United
 ambae pia yumo Timu ya Taifa ya Netherlands, alieleza: “Yapo matukio 
mazoezini ambapo Wachezaji hutofautiana. Mnayazungumza. Na hivyo ndivyo 
ilivyokuwa na yamekwisha.” Blind pia alisisitiza kuwa tukio hilo halikumfanya ampige Benchi Van Persie kwenye Mechi na Kazakhstan ambayo aliingizwa Kipindi cha Pili na kufikisha Mechi 100 kwa Nchi yake.
Pia
 Van Persie, ambae aliihama Man United Mwezi Julai kwenda Fenerbahce ya 
Uturuki ukiwa ni Mwezi mmoja tu baada ya Depay kuhamia Man United, ndie 
Mfungaji Bora wa Holland katika Historia ya Nchi hiyo akiwa na Bao 49.
0 maoni:
Chapisha Maoni