Arsenal Mabingwa 2015 FA Community Shield
Alex Oxlade akipeta baada ya kufunga bao
Chamberlain akishangilia vikali juu kwa juu
Mbele ya Mashabiki
Msimu
mpya wa Soka huko England umeanza rasmi hii Leo kwa Mechi maalum ya
kugombea Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa wa England Chelsea na waliobeba
FA CUP Arsenal Uwanjani Wembley Jijini London na Arsenal kuibuka kidedea
kwa kuifunga Chelsea 1-0 ikiwa ni ishara maalum Msimu huu wametangaza
nia ya kutwaa Ubingwa. Huu ni ushindi wa kwanza kwa Arsenal, chini ya Meneja Arsene Wenger, dhidi ya ya Chelsea, chini ya Meneja Jose Mourinho, ambao washakutana uso kwa uso mara 13 na Chelsea kushinda mara 7 na Sare 6.
Alex Oxlade-Chamberlain alifunga Bao pekee na la ushindi kwa Arsenal katika Dakika ya 24 alipopokea pande zuri toka kwa Theo Walcott na hilo ni Bao la kwanza kabisa dhidi ya Chelsea, chini ya Meneja Jose Mourinho, tangu 2007.
Alex Oxlade Chamberlain akipongezwa
Cazorla na Chamberlain
Kocha wa Timu ya Chelsea Jose Mourinho akijionea Vijana wake Wembley
Theo Walcott akigombea mpira wa Kichwa dhidi ya kipa wa Chelsea
Monreal nae kwenye patashika mpira wa kichwa
Chupuchupu langoni mwa Arsenal Petr Cech akiokoa
0 maoni:
Chapisha Maoni