.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 20 Julai 2015

Tagged Under:

THE STARS BAND YAZINDULIWA RASMI SIKU YA EID MOSI NDANI YA MZALENDO PUB HUKU IKISINDIKIZWA NA BENDI YA FM ACADEMIA PAMOJA NA BARNABA

By: Unknown On: Jumatatu, Julai 20, 2015
  • Share The Gag



  • Bendi mpya ya muziki wa dansi ijulikanayo kama The Stars Band iliyo chini ya Aneth Kushaba imezinduliwa rasmi siku Jumamosi ya Julai 18, siku ya Idd-Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku ikisindikizwa na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Barnabas pamoja na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

    Mkurugenzi wa The Stars Band, Aneth Kushaba akijitambulisha kwa mashabiki wakenm pamoja na azungumza na wapenzi wa bendi mpya ya The Stars Band wakati wa uzinduzi yeye binafsi alisema hawezi kusema yaliyopita bali wapenzi wa bendi hiyo wategemee makubwa kutoka kwenye bendi hiyo iliyozinduliwa siku ya Idd Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub

    Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Felly Kano akionesha mambo yake kwenye stage hii yote ni wakati anajitambulisha kwa mashabiki wa bendi waliofika kwenye uzinduzi wa bandi hiyo

    Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Seghito mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangozi akijitambulisha kwa kuonesha uwezo wake kwenye stage wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika katika kiota cha Mzalendo Pub jijini Dar

    Mpiga Drums na pia ndiye meneja wa Bendi, Kibosho akijitambulisha kwa kuone uwezo wake katika Drums

    LOUIS VAN GAAL: MASTRAIKA WANATOSHA KWA SASA!

    Kocha mkuu wa Manchester United Louis Van Gaal ametamba kuwa hatanunua mshambuliaji mwingine kwani alio nao kwa sasa wanatosha wakiongozwa na Wayne Rooney.
    Pamoja na Wayne Rooney washambuliaji wengine waliobaki ni Javier Hernandes Chicharito, na James Wilson baada ya mshambuliaji mpachika magoli Robin Van Persie kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki hivi karibuni na Radamel Falcao mkopo wake kumalizika.

    Van Gaal anatarajia kumtumia Rooney kama mshambuliaji pekee pale mbele ambapo atasaidiwa na Mephis Depay aliyesajiliwa wakati wa majira ya joto kutoka PSV Eindhovenya Uholanzi.
    Van Gaal anatamba kuwa Depay anaweza kuwa mshambuliaji wa katikati tofauti na alivyokuwa akitumika wakati alipokuwa PSV.

    UHAMISHO: KIPA SERGIO ROMEO ATAKIWA OLD TRAFFORD!

    Manchester United wananyemelea kumsaini Kipa Sergio Romero wakati Meneja wao, Louis van Gaal, akisaka kumbadili Victor Valdés anaeuzwa.
    Romero, mwenye Miaka 28, Msimu uliopita alikuwa kwa Mkopo huko AS Monaco kutoka Sampdoria na kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka Jana, Kipa huyo aling'ara alipokuwa Namba Wani wa Argentina iliyofika Fainali na kufungwa 1-0 na Germany.
    Hata hivyo, AS Roma nayo pia inamtaka Romero ambae sasa ni Mchezaji Huru baada ya Mkataba wake na Sampdoria kumalizika.
    Van Gaal anamtaka Romero kuziba pengo la Valdés ambae alikwaruzana nae kwa kugomea kuchezea Kikosi cha Pili cha Man United na hilo kumfanya asichukuliwe kwenye Ziara ya sasa huko Marekani.

    Man United pia ina uwezekano wa kumpoteza Kipa wao Namba Moja, David de Gea, anaetakiwa kwa udi na uvumba na Klabu ya Nchini kwao Spain, Real Madrid.
    Hata hivyo, Sergio Romero anatarajiwa kuwa Kipa Namba Mbili nyuma ya Kipa yeyote atakaembadili De Gea, ikiwa ataondoka, huku Kipa wa Ajax na Timu ya Taifa ya Holland, Jasper Cillessen, akitajwa kuwa ndie mrithi wa De Gea.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni