




Morgan Schneiderlin Anaipachikia bao la mapema la kichwa na kufanya 1-0 dhidi ya Club America katika dakika ya 5 baada ya kusaidiwa na Juan Mata aliyeunganisha mpira wa kona na kumpata Morgan. Schneiderlin anaanza vyema Man United!
Hadi Mapumziko Manchester United 1 Club America 0. Kipindi cha pili kiliendelea vyema na Kocha kabla ya Mechi hii, Meneja wa Man United Louis van Gaal alisema atachezesha Timu mbili na kweli alifanya hvyo baada ya kubadili Wachezaji 11 kwa ajili ya Kipindi cha Pili.

Wachezaji 11 walioingizwa Kipindi cha Pili ni Kipa Lindegaard, McNair, Smalling, Evans, Blackett, Schweinsteiger, Herrera, Lingard, Pereira, Januzaj, Wilson.


Schneiderlin akipongezwa na Phil Jones pamoja na Memphis Depay

Wayne Rooney na Pablo Cesar Aguilar






Man United XI: Johnstone, Darmian, Jones, Blind, Shaw, Carrick, Schneiderlin, Young, Mata, Memphis, Rooney
Club America: Gonzalez, Mares, Aguilar, Sambueza (c), Goltz, Arroyo, Samudio, Guemez, Quintero, Martinez, Buron
Mashabiki: 48,857
0 maoni:
Chapisha Maoni