.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 16 Julai 2015

Tagged Under:

SERIKALI KENYA YAOKOA USHIRIKI WA GOR MAHIA KOMBE LA KAGAME, SASA YANGA WAJIPANGE

By: Unknown On: Alhamisi, Julai 16, 2015
  • Share The Gag



  • SERIKALI ya Kenya imeipiga jeki Gor Mahia iweze kuja Dar es Salaam kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya mkwamo uliotishia ushiriki wao.
    Serikali imeisaidia Gor tiketi 30 za ndege kuja Dar es Salaam na kurudi Nairobi baada ya mashindano- ambayo yataanza Jumamosi.
    Gor ilikuwa katika hatihati ya kuja kushiriki Kagame, baada ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF), kugoma kuwapa tiketi wakisema hilo si jukumu lao. 
    “Tumepokea msaada wa Serikali kupitia Wizara ya Michezo Sanaa na Utamaduni, wametupa tiketi za kwenda na kurudi wenye mashindano na tumefarijika. Sasa tuko tayari kwenda”, amesema Katibu Mkuu Msaidizi wa Gor, Ronald Ngala akihojiwa na Futaa.com mjini Nairobi.
    Gor Mahia wanakuja Dar es Salaam kwa msaada wa Serikali ya Kenya

    Gor imepangwa Kundi A pamoja na wenyeji wengine, Yanga SC, Telecom ya Djibout, KMKM ya Zanzibar na Khartoum-N ya Sudan na Kundi B kuna APR ya Rwanda, Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi, Heegan FC ya Somalia wakati Kundi C kuna wenyeji wengine, Azam FC, Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.
    Gor watamenyana na Yanga SC kuanzia Saa 10:00 jioni Jumamosi baada ya APR ya Rwanda kupepetana na Al Shandy ya Sudan katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, kuanzia Saa 8:00 mchana.
    Mchezo mwingine wa siku hiyo, utafanyika Uwanja wa kumbukumbu ya Karume, Ilala ukizikutanisha KMKM na Telecom ya Djibouti kuanzia Saa 10:00 jioni.
    Waziri wa Miundombinu nchini Tanzania, John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano hiyo Julai 18 Uwanja wa Taifa.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni