Louis van Gaal amekiri Javier Hernandez 'Chicharito'
atapata nafasi nyingine ya kupigania nafasi yake kwenye Kikosi cha
Manchester United akiungana na Timu hiyo hapo Julai 25 huko Ziarani
Marekani. Chicharito, ambae aliifungia Man United Bao 59 katika Mechi154, alipelekwa kwa Mkopo huko Real Madrid Msimu uliopita baada Van Gaal kuamua atakuwa nyuma ya Wayne Rooney, Robin van Persie na Radamel Falcao katika kupewa namba.

Lakini, baada ya Man United kuifunga Club America 1-0 mapema Leo, Van Gaal aliulizwa hatima ya Chicharito na kueleza: "Chicharito anakuja Julai 25. Ana nafasi ya kudhihirisha uwezo wake hasa baada ya Falcao na Van Persie kuondoka, hivyo nafasi yake kubwa."
Hivi
sasa Man United imebakiwa na Mastraika Wawili tu wanaotambulika ambao
ni Kepteni Wayne Rooney na James Wilson na alipoulizwa kuhusu upungufu
huo, Van Gaal alijibu: "Hapana tunae Rooney anaweza kucheza kama Straika
mkuu. Wanahabari wote Msimu uliopita waliandika anapaswa kucheza hapo
na mimi nawasikiliza. Na tunae Chicharito, na labda Wilson, na pengine
kwa kushangaza..mpya., huu ni mchakato. Sina wasiwasi na nafasi hiyo."
0 maoni:
Chapisha Maoni