.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 21 Julai 2015

Tagged Under:

Mourinho analaumu FC Porto kumsajili Casillas pamoja na mshahara wake?

By: Unknown On: Jumanne, Julai 21, 2015
  • Share The Gag

  • jose-mourinho-chelsea_e5smuyx0q03h1346wwab0ldj5
    Iker Casillas amelelewa na Klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa miaka 25, ndani ya kipindi hicho ameichezea Klabu hiyo kwa miaka 16, lakini mambo yakabadilika baadae ambapo mwezi huu alitangaza kuhamia Klabu ya FC Porto ya Ureno kwa mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi.
    Casillas amejiunga na FC Porto na atakuwa analipwa mshahara wa pound milioni 1.7 kwa mwaka.
    mou-kicks-iker-514
    Hata hivyo kufuatia uhamisho huo kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amelaumu uamuzi wa FC Porto kumsajili kipa wa Real Madrid Iker Casillas kwa mkataba wa muda mrefu na wenye maslahi mazuri… Mourinho ambaye aliwahi kuwa kocha wa Real Madrid kati 2010 hadi 2013 hana imani na uwezo wa Casillas kuna wakati aliwahi kumuweka benchi na nafasi yake kumpa Diego Lopez.
    Iker19495000
    Lakini pia Mourinho alishangazwa na maamuzi mengine ya FC Porto kumsajili kiungo kutokea klabu ya Marsseille ya Ufaransa Giannelli Imbula kwa dau la pound milioni 13.8.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni