Timu
zote zinazoshiriki michuano ya Kombe la Kagame zinatakiwa kufika mjini
Dar es Salaam si zaidi ya leo tarehe 16 mwezi wa saba tayari kwa kuanza
kipute jumamosi. Kwa hivyo bila shaka hii leo kufikia jioni vikosi vyote
vya timu 13 vitakuwa vimefika nchini Tanzania. Timu zote zinatakiwa
kujilipia gharama za usafiri huku mambo mengine yakifanywa na waandaaji.Na kama ndiyo kwanza unasikia basi fahamu tu kuwa vilabu 13 kutoka ukanda wa Afrika masharik na kati vitakuwa vikichuana ili kuutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame ambalo linaenda sambamba na mgawanyo wa dola elfu 60 za kimarekani kutoka kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame. Tayari Timu ya wanamichezo wa BBC imeanza kuifuatilia michuano hiyo na tutakuletea mambo yote.
0 maoni:
Chapisha Maoni