.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 3 Julai 2015

Tagged Under:

KUTOKA KWA MENEJA BEPPE MAROTTA - PAUL POGBA NI NGUMU KUMWACHIA HUKU BARCELONA WAKITAKA KUMNUNUA KWA KITITA CHA MILLIONI 80!

By: Unknown On: Ijumaa, Julai 03, 2015
  • Share The Gag


  • Paul Pogba
    Mgombea wa wadhfa wa urais katika klabu ya Barcelona Joan Laporta anasema kuwa mabingwa hao wa Ulaya watajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Juventus Paul Pogba iwapo atachaguliwa.
    Ripoti zinasema kuwa kilabu ya Barcelona ilijaribu kumsajili raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 ambaye aliisaidia Juventus kushinda ligi ya Serie A na kufika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.
    ''Kuna mchezaji tunayempenda sana -Paul Pogba. Tunamjua ajenti wa mchezaji huyo na hilo na swala muhimu katika oparesheni zetu. Tutajadiliana na wakala wake pamoja na klabu ya Juventus'',. Alisema Laporta.

    Siku ya Jumatano, Vyombo vya habari Nchini Uhispania na Italy vilisema kuwa Barcelona imetoa kitita cha yuro milioni 80 kwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United ambaye pia anahusishwa na uhamisho katika vilabu vya Chelsea na Manchester City.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni