.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 6 Julai 2015

Tagged Under:

Drogba kawataja hawa mabeki kwamba ndio waliomsumbua zaidi Uwanjani.

By: Unknown On: Jumatatu, Julai 06, 2015
  • Share The Gag
  • Didier-Drogba-Wallpaper_0
    Didier Drogba
    Gwiji wa zamani wa soka la kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Chelsea, Didier Drogba, ni mmoja wa washambuliaji bora zaidi waliowahi kutamba katika barani Afrika, Asia na Ulaya.
    Galatasaray's Didier Drogba
    Drogba ambaye alitangaza kustaafu kuichezea Ivory Coast mwaka jana, pamoja kufahamika kuwa mwiba mkali kwa mabeki wa timu pinzani wakati akiwa kwenye ubora wake, Drogba pia nae alikuwa na mabeki ambao walikuwa ni visiki zaidi kila alipokuwa anakutana nao.
     
    Didier Drogba amemtaja nahodha wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Spain, Carles Puyol, Rio Ferdinand, na Nemanja Vidic kuwa ndio mabeki visiki zaidi aliowahi kukutana nao.
    Akizungumza katika mahojiano yake na Rio Ferdinand, Didier Drogba alisema.
     
    “Siku zote nimekuwa nikisema wewe Rio na Vidic ni walinzi ambao nilikuwa napata sana taabu timu zetu zinapokutana… Nilipokuwa nikifunga dhidi ya Manchester United nilikuwa nafurahia sana kwa sababu si mara nyingi nilikuwa nikipata nafasi ya kufunga dhidi yao.”

    0 maoni:

    Chapisha Maoni