Manchester United ndio Nambari Wani kwa kuwa ndio bidhaa yenye thamani kubwa zaidi miongoni mwa Klabu za Soka Duniani. Licha ya kutotwaa Taji lolote Msimu uliopita, Man United imeiengua Bayern Munich na kukamata Nafasi ya Kwanza kwa kuwa ndio Bidhaa ya Biashara yenye thamani kubwa ikikadiriwa kuwa ni Dola Bilioni 1.2 na hii ni kwa mujibu wa takwimu za Washauri mahsusi wa Bidhaa na Fedha, Brand Finance.
Katika Listi iliyotolewa na Washauri hao wa Bidhaa na Fedha, Klabu 6 katika 10 Bora Duniani ni za England.
Barcelona, ambao Juzi Jumamosi walitwaa Kombe la UEFA CHAMPIONS LIGI, wameporomoka Nafasi 2 na sasa wapo Nafasi ya 6.
Ingawa
Magazeti ya Spain yamekuwa yakivutia upande wa Klabu zao na kudai Man
United, kwa kukosa Mataji, imepoteza Mashabiki wengi Duniani, Ripoti ya
Brand Finance imesema: "Hata kama ripoti hizo za kupoteza Mashabiki
itaaminika, Man United bado ina Maelfu ya Washabiki huko India, Kusini
Mashariki ya Asia na China, ikijumuisha zaidi ya Nusu Bilioni ya Watu na
habari hizo hazijawakimbiza Wadhamini." Brand Finance imesema kuwa kwa kusaini Dili na Wadhamini kama Chevrolet na Adidas, ambao walisaini nao 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 750 kwa Miaka 10, ni vitu tosha kuthibitisha thamani ya Klabu hiyo na kwamba thamini yao itapanda zaidi kama ilivyopanda kwa Asilimia 63 tangu 2014.

KLABU 20 BORANA THAMANI YAKE!
1. Manchester United (England): $1206 Milioni
2. Bayern Munich (Germany): $933 M
3. Real Madrid (Spain): $873 M
4. Manchester City (England): $800 M
5. Chelsea (England): $795 M
6. Barcelona (Spain): $773 M
7. Arsenal (England): $703 M
8. Liverpool (England): $577 M
9. Paris Saint-Germain (France): $541 M
10. Tottenham Hotspur (England): $360 M
0 maoni:
Chapisha Maoni