.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 24 Aprili 2015

Tagged Under:

YANGA SC VS RUVU SHOOTING. LEO HIII

By: Unknown On: Ijumaa, Aprili 24, 2015
  • Share The Gag

  • VINARA wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga, Ijumaa wanaingia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting wakijua ushindi Mechi hii na mwingine hapo Jumatatu dhidi ya Polisi Moro utawapa Ubingwa huku wakiwa na Mechi 2 mkononi.

    Hivi sasa Yanga wako kileleni wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 22 wakifuatiwa na Mabingwa Watetezi Azam FC wenye Pointi 42 kwa Mechi 22 na Simba wapo Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 38 kwa Mechi 23.
    Hivyo Yanga, ambao tayari wameshakuwa moja ya Timu mbili zitakazocheza Mashindano ya CAF ya Klabu Barani Afrika Msimu ujao, wanahitaji Pointi 6 tu kuwa bila Bingwa bila kujali nini mpinzani wake Azam FC anakifanya.

    Hata hivyo, Yanga wana wakati mgumu hivi sasa baada ya kukabiliwa na Majeruhi kwenye Difensi yao kwa kuwakosa Kepteni Nadir Haroub 'Cannavaro' na Kevin Yondani pengo ambalo Juzi lilishuhudia Stand United kuwaendesha mchakamchaka na kushinda kwa mbinde 3-2.
    Azam FC Jumamosi wanacheza Nyumbani kwao na Stand United na ili kuweka uhai matumaini yao finyu ya kutetea Taji watalazimika kushinda tu kitu ambacho pia kitawasaidia kukwepa Simba, ambao Jumatano waliitwanga Mgambo JKT 4-0, kuwapiku Nafasi ya Pili.

    LIGI KUU VODACOM
    RATIBA:

    Leo Ijumaa Aprili 24
    Ruvu Shooting v Yanga
    Jumamosi Aprili 25
    Mbeya City vs Kagera City
    Simba vs Ndanda FC
    Azam FC vs Stand United

    0 maoni:

    Chapisha Maoni