.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 16 Aprili 2015

Tagged Under:

KLABU AFRIKA: ETOILE DU SAHEL KUTUA JIJINI DAR, Y

By: Unknown On: Alhamisi, Aprili 16, 2015
  • Share The Gag

  • Yanga, Wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia kwenye michuano ya Klabu Barani Afrika, Jumamosi wapo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Etoile du Sahel ya Tunisia katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.Yanga imetua hatua hii baada ya kuzibwaga BDF XI ya Botswana na FC Platinum ya Zimbabwe katika Raundi za awali.
    Akizungumzia Mechi hii, Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema ni muhimu kushinda Mechi hii ya Nyumbani na pia kuwa makini na staili ya kupoteza muda ambayo Etoile du Sahel wanategemewa kuitumia.Yanga inatarajiwa kuwatumia tena Wachezaji wao muhimu ambao walikuwa Majeruhi ambao ni Salum Telela na Coutinho.
    Etoile du Sahel inatarajiwa kutua Dar es Salaam leo hii kwa Ndege ya kukodi.

    CAF KOMBE LA SHIRIKSHO
    Mechi za Kwanza Raundi ya Mtoano ya Timu 16
    Mechi kuchezwa Wikiendi ya Aprili 18

    Association Sportive Olympique de Chlef vs Club Africain
    Djoliba AC vs Hearts of Oak
    Young Africans vs E.S. Sahel
    Royal Leopards vs AS Vita Club
    Onze Createurs vs ASEC Mimosas Abidjan
    Warri Wolves vs Etanchéité
    CF Mounana vs Orlando Pirates
    Al Zamalek vs Fath Union Sport de Rabat

    Marudiano Wikiendi ya Mei 5

    Washindi 8 wa Raundi hii watajumuika na Timu 8 zilizobwagwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na kuwekwa kwenye Droo maalum kupanga Mechi 8 za Mtoano na Washindi wake 8 kutinga hatua ya Makundi ambayo yatakuwa na Makundi mawili ya Timu 4 kila mmoja yatakayocheza Mtindo wa Ligi wa Nyumbani na Ugenini.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni