Ligi
kuu Tanzania Bara itaendelea wikiendi hii huku kocha wa mabingwa wa
zamani wa Tanzania Bara, Simba, Mserbia Goran Kopunovic akiipigia
mahesabu ya ushindi timu ya Kagera Sugar katika uwanja wa Uwanja wa CCM
Kambarage Mjini Shinyanga ambao wanautumia kama uwanja wao wa Nyumbani
baada ya ule wa Kaitaba kuwa kwenye Matengenezo. Mchezo huo unatarajiwa
kuchezwa hapo Jumamosi kesho kutwa.
Simba
ina pointi 32, ikiwa ya tatu katika msimamo, ambapo wapinzani wao wa
jadi, Yanga wanaongoza Ligi wakiwa na pointi 40 huku Azam wakiwa nafasi
ya pili na pointi 36.
0 maoni:
Chapisha Maoni