Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers kutoka Mjini Bukoba leo kimefanya Tamasha kubwa la Pasaka kwenye Mji wa Geita katika Ukumbi wa GEDECO na kushuhudiwa na Umati wa Watu wengi zikiwemo Kwaya mbalimbali za hapa Geita na Waumini mbalimbali na kuifurahia Pasaka hiyo ambayo ni Alama ya Ukombozi wa Mwanadamu dhidi ya Dhambi kupitia kifo na Ufufuko wa Yesu Kristo. Wana'KAPOTIVE walisindikizwa na kwaya ya Mt. Thomas wa Aquino na Aaron Entertainment wa hapo Geita. Watu walivutiwa sana na kiwango cha juu ya kikundi cha KAPOTIVE mpaka wengine wakadiriki kusema sio kutoka Bukoba.
Watu hawakuweza kujizuia na kuanza kujimwaga kwa muziki wa Yesu, palikuwa hapatoshi!!!!
Vijana
machachari wa Kapotive Star Singers, Denis Deus na Claudius Mutabuzi
wakilikamatilia jukwaa kwa mbwembwe zote ilimradi kuwakamata watazamaji
waliofurika ukumbi wa GEDECO.
Mambo si ndo hayo!!!!
0 maoni:
Chapisha Maoni