.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 3 Aprili 2015

Tagged Under:

BRENDAN: RAHEEM STERLING KUBAKI LIVERPOOL, HAONDOKI KOKOTE MWISHONI MWA MSIMU! APASHA NA WENZAKE KUJIANDAA KUIANGUSHA ARSENAL JUMAMOSI!

By: Unknown On: Ijumaa, Aprili 03, 2015
  • Share The Gag

  • Raheem Sterling na Daniel Sturridge wakifurahia jambo wakati wa mazoezi kujiandaa na Mtanange wa Ligi Kuu England kati yake na Arsenal.

     
     Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers nae amesema mchezaji huyo kubaki Liverpool, Haendi kokote!! Bosi wa Brendan Rodgers amesema Fowadi wa Liverpool Raheem Sterling hataondoka mwishoni mwa Msimu licha ya mazungumzo ya Mkataba mpya kati yake na Klabu kuvunjika.
    Juzi Sterling, Kijana wa Miaka 21, akifanya Mahojiano na BBC, alisema kuukataa Mkataba mpya ambao ungemlipa Pauni 100,000 kwa Wiki badala ya 35,000 za sasa si uroho wa Fedha Bali nia yake yeye na kutwaa Mataji.
    Zipo ripoti kuwa Sterling yuko mbioni kuhamia Barcelona au Real Madrid Klabu za Spain lakini pia habari hizo zimegusia kubaki kwake England Ila atahamia Chelsea au Arsenal.
    Mario nae alikuwemo mazoeziniMazoezi yakiendelea...Hapo Jana Brendan Rodgers amesema: "Liverpool no Mona ya Supapawa za Soka. Wamiliki wakisema hauzwi Mchezaji, basi hauzwi!"
    Katika Mkataba wake was sasa na Liverpool, Sterling amebakisha Miaka Miwili.
    Rodgers pia alisema Raheem, ambae alijiunga na Liverpool 2010 akitokea QPR, hakuruhusiwa kufanya Mahojiano na BBC lakini atajifunza kutokana na makosa take.

    Pia Wachambuzi wengi was Soka huko Uingereza wameibuka na kumtaka Sterling abakie Liverpool kwani hajakomaa Kisoka kwenda nje.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni