.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 24 Aprili 2015

Tagged Under:

SEVILLA, NAPOLI, FIORENTINA NA DNIPRO HAO WAINGIA NUSU FAINALI!!

By: Unknown On: Ijumaa, Aprili 24, 2015
  • Share The Gag

  • UROPA LIGI, Mashindano makubwa ya pili kwa Klabu Barani Ulaya, Usiku huu Alhamisi yamemaliza Mechi zake za Robo Fainali na Mabingwa Watetezi Sevilla ya Spain, Dnipro Dnipropetrovsk ya Ukraine na Timu mbili za Italy, Fiorentina na Napoli, zimefuzu kuingia Nusu Fainali.
    FIORENTINA 2 vs 0 DYNAMO KIEV
    Fiorentina wamefuzu kuingia Nusu Fainali ya EUROPA LIGI baada ya kuitandika Dynamo Kiev Bao 2-0 na kusonga kwa Jumla ya Bao 3-1 katika Mechi mbili.

    Mchezaji wa Fiorentina Mario Gomez akiziona nyavu za wapinzani wao usiku huu. Gomez akishangilia pamoja na mwenzake Marcos Alonso baada ya Fiorentina kusonga hatua ya Nusu Fainali
    Jeremain Lens wa Dynamo alipewa Kadi Nyekundu Dakika ya 40 baada ya kulambwa Kadi ya Njano ya Pili kwa kujiangusha kwa makusudi kwenye Boksi la Fiorentina.
    Dakika 3 baadae Mario Gomes akaipa Fiorentina Bao na wakapiga Bao la Pili Dakika ya 90 kupitia Juan Manuel Vargas.

    NAPOLI 2 vs 2 WOLFSBURG
    Napoli wameingia Nusu Fainali ya EUROPA LIGI baada ya kutoka Sare 2-2 na Wolfsburg na kufuzu kwa Jumla ya Mabao 6-3 kufuatia ushindi wao wa 4-1 wa Ugenini huko Germany Wiki iliyopita.
    Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0 lakini Napoli waliingia Kipindi cha Pili wakiwa moto na kufunga Bao 2 katika Dakika za 50 na 65 kupitia Jose Callejon na Dries Mertens.

    Dakika ya 71 Wolfsburg walipata Bao Mfungaji akiwa Timm Klose na Dakika 2 baadae Ivan Perisic aliifanya Gemu kuwa 2-2.
    DNIPRO 1 vs 0 CLUB BRUGGE
    Kufuatia Sare ya 0-0 Ugenini, Dnipro wakicheza kwao walishinda 1-0 na kuingia Nusu Fainali ya EUROPA LIGI.
    Dnipro walipata Bao lao la ushindi Dakika ya 83 Mfungaji akiwa Yevgeniy Shakhov.


    ZENIT 2 vs 2 SEVILLA

    Mabingwa Watetezi wa EUROPA LIGI, Sevilla, wakicheza Ugenini huko Urusi, walitoka Sare 2-2 na Zenit lakini wamefuzu kwa Jumla ya 4-3.

    Sevilla walifunga Bao la kwanza kwa Penati ya Carlos Bacca Dakika ya 5 kufuatia Rafu ya Neto na Zenit kurudisha Dakika ya 48 baada Kipa Beto kuutema Mpira na Jose Salomon Rondon kufunga na kisha kwenda 2-1 mbele kwa Bao la Hulk la Shuti la mbali katika Dakika ya 72.
    Sevilla walipata Bao muhimu Dakika ya 85 kupitia Kevin Gameiro na Gemu kuwa 2-2.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni