Aslay
Isihaka maarufu kwa jina la ‘Dogo Aslay’ na Bakari Abdul katuti ‘Beka’
wakiimba Moja ya Wimbo wao kwenye Ukumbi wa "Rest House" ukumbi wa
Jeshi Wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera kwenye Shoo yao iliyoweza
kushuhudiwa na Mashabiki wengi wa Muziki huo wa Bongo Flava katika
Ukumbi huo Biharamulo. Shoo hiyo ilifanyika Usiku wa tarehe 07.04.2015
katika Siku maalum ya Hitma ya kumkumbuka Hayati, Muasisi wa Mapinduzi
Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ambayo ilipewa jina la "Karume
Day".
Nyimbo
kibao ikiwemo NITAJUTA, NISEME, WAMBEA, NITAKUPWELEPWETA ziliimbwa
katika Ukumbi huo wa Rest House ambao ni Ukumbi wa Jeshi katika Mji huo.
Yamoto Band unakuwa umegusa majina ya Vijana Machachari wanne ambao
ni Waimbaji wenye Sauti Tamu na Vipaji vya hali ya juu kutoka Mikoa
tofauti hapa Nchini Tanzania. Kundi hilo ambalo lilianza kuunguruma
katika Mji wa Mwanza, Geita, Bukoba Mjini na pia kumalizia Burudani zake
hapa Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera na Vinaja hao kufanya vyema
katika Miji hiyo.

Aslay na mwenzake wakiwajibika vilivyo jukwaani

Kundi hilo linaundwa na Aslay Isihaka maarufu kwa jina la ‘Dogo Aslay’,
Mbwana Yusuph Kilungi ‘Maromboso’, Enock Deogratius ‘Enock Bella’ pamoja
na Bakari Abdul katuti ‘Beka’.

Hakika ilikuwa Burudani

Nyomi ya kutosha usiku huo

‘Dogo Aslay’, Mbwana Yusuph Kilungi ‘Maromboso’ wakiwajibika Jukwaani
Maromboso akifanya yake kwa Mashabiki wao

Jerry kwenye picha akitokelezea na mashabiki

Kiongozi Mnec (kulia) Bw. Yusuph A. Khatry akiwa na Mama

Sunday(kulia)
katikati ni Jonathan Mwanga --Waandaaji wa Shoo hiyo wakiwa na Rafiki
yao kikazi Bw. Willy Kiroyera ambaye walikutana nae usiku huo wa shoo
akitokea Nchi jirani ya Rwanda mjini Bujumbura kwenye shughuli za
kitalii.

Wadau..wakifuatilia Muziki huo kwa makini..

Willy O. Rutta akipeana neno na Mtangazaji wa Radio Kasibante Fm Bw.
Abdulrazak Majid(kulia) wakati wa Shoo hiyo ya Yamoto Band Biharamulo.

Wadau

Machote yote kwa Waimbaji wa Kundi la Yamoto Band.


Nani zaidi!!

Mashabiki wakiyarudi mangoma ya Live kutoka kwa Yamoto Band


Shabiki wa Yamoto Band nae akijinafasi mbele ya Mashabiki wenzake

Mambo ya Yamoto Band

Hatari sana! Burudani ikiendelea..

Bw. Jonathan Mwanga akipata ukodak na Shabiki wake Biharamulo usiku huu.


Dada moja wa waimbaji Chipukizi wa Said Fella Getrude akiwajibika jukwaani kwa kufokafoka Rap

Baadhi
ya Mashabiki waliohudhuria katika shoo ya bendi ya YAMOTO katika
ukumbi wa Rest House jana usiku wakionekana kumkubali Dada huyo mkali wa
Kurap .

Chiba akifanya yake huku akiwa kasimama kwa mguu mmoja pekee

Kipaji ni kipaji

Waimbaji
wanaounda kundi la “Yamoto Band”Aslay, Becka, Bella na Maromboso
wakitoa burudani sambamba na Kijana wao mwenye mguu mmoja Chiba"
0 maoni:
Chapisha Maoni