Meneja
wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa Mchezaji wao Raheem Sterling
hakuonyesha nidhamu ya Mwanamichezo baada ya kuibuka Picha akivuta
Mtemba maarufu kama Shisha ambao unadhaniwa kuwa na Gesi inayolewesha
'Nitrous Oxide.'
Picha
za Sterling akivuta Shisha zilizagaa Jana huko England kwenye Vyombo
vya Habari na baadae kuibuka Picha nyingine zikimwonyesha Staa huyo wa
Miaka 20 ambae pia huchezea England akiwa 'amezimika.' Akiongea
mara baada ya Jana Liverpool kuifunga Newcastle 2-0 na kupanda hadi
Nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England huku Sterling akifunga Bao la
kwanza, Rodgers amesema: "Ukiwa Mwanamicheza wa kiwango cha juu hupaswi
kufanya hivyo. Nitaongea nae na kumsikia anasemaje." Rodgers amekiri kuwa Wachezaji Vijana Siku zote hufanya makosa lakini kikubwa ni kujifunza toka makosa hayo.
0 maoni:
Chapisha Maoni