Robin van Persie amejitangaza kuwa yupo vizuri kwa mchezo wa jumapili dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester city.Van Persie amekosekana michezo sita ya Manchester united kutokana na kuumia enka wakati Man Utd walipopoteza kwa 2-1 dhidi ya Swansea tarehe 21 mwezi wa pili.
Kocha
Louis van Gaal wiki iliyopita alisema hakutegemea Van Persie kupona kwa
haraka hivyo na kua vizuri kupambana na city jumapili ijayo pale Old
Traffod,lakini Van Persie mwenyewe alijitangaza kwa mashabiki na
kuwaambia yupo vizuri.
Hata
kama van Gaal akifikiria kumpa nafasi katika mechi yao ya upinzani wa
jadi dhidi ya city bado ni ngumu sana kuona jinsi gani ataendana na kasi
na mfumo wa sasa ya kitika kikosi cha kwanzaPengo la mholanzi ambae amefunga magoli 10 tu msimu huu halikuonekana kabisa pale alipoumia,na tangu alipoumia man united imepoteza mchezo mmoja tu tena dhidi ya mabosi wake wa zamani Arsenal kombe la FA.
United
walipata ushindi katika ratiba ngumu dhidi ya Tottenham na Liverpool na
jumamosi iliyopita ushindi wa 3-1 dhidi ya Aston Villa ushindi
uliofanya kuwa juu ya city kwa pointi moja.
Wayne
Rooney alifunga goli moja matata kwa mkwaju wa haja,kapteni huyo wa
united amekua na kiwango bora kabisa pale mbele katika mfumo wa 4-3-3
akisaidiana na Ashley Young na Juan Mata ambae aliingia nyavuni mara
mbili katika ushindi wa 2-1 pale Anfield wiki mbili na nusu zilizopita.
Marouane
Fellaini pia anatoa mchango mkubwa katika majukumu ya kiungo na
ushambuliaji sehemu ambayo kwa sasa imetulia sana kwenye kikosi hicho
cha Manchester united.
Ushindi
dhidi ya city iliyopoteza mwelekeo na kuwa chini ya kiwango utaongeza
wigo wa pointi kufikia nne na kuongeza matumaini ya Van Gaal kucheza
ligi ya mabingwa msimu ujao.
Mata na Ander Herrera
0 maoni:
Chapisha Maoni