.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 11 Aprili 2015

Tagged Under:

JUMAPILI:MANCHESTER UNITED vs MANCHESTER CITY

By: Unknown On: Jumamosi, Aprili 11, 2015
  • Share The Gag


  • Wachezaji wa Manchester United wakijifuia leo Ijumaa tayari kwa Dabi yao ya Jumapili na Manchester City

    Meneja Louis van Gaal akiangalia Vijana wake wanavyojituma kwenye mazoezi leo hii
    Kipa David de Gea, Angel di Maria na Straika Radamel Falcao kwenye mazoezi leo

    Straika Robin van Persie ameshatangaza kwa wadau kwamba katika kipute hicho cha Manchester atakuwepo na anategemea kucheza mchezo huo dhidi ya Manchester City
    Falcao na Antonio Valencia
    Nahodha wa Man United kwa sasa Rooney kuiongoza Debi hiyo Siku ya Jumapili dhidi ya City

    Van Gaalakitathimini mazoezi hayo na akijiuliza juu ya mchezo huo wenye Upinzani mkali

    Rooney, Ashley Young, goalkeeper Anders Lindegaard na Michael Carrick
    NAHODHA wa Manchester United Wayne Rooney ameieleza Dabi ya Manchester ya Jumapili hii kuwa ni Gemu kubwa ya kuleta kiburi. Jumapili, Manchester United watakuwa kwao Old Trafford kuwakaribisha Mahasimu wao kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ambayo inazikutanisha Man United iliyo Nafasi ya 3 Pointi 1 mbele ya City ambayo iko Nafasi ya 4.
    Rooney, ambae ameshapiga Bao 11 kwenye Dabi ya Manchester akishikilia Rekodi ya Kihistoria ya kufunga Bao nyingi kwenye Dabi hii, amesema anataka Mashabiki wa Man United wakienda Makazini kwao Jumatatu wawacharure wale wa City.
    Lakini hivi karibuni City ndio wamekuwa wakiiburuza United kwa kushinda Mechi 4 mfululizo ingawa Kihistoria hakuna hata Timu moja iliyowahi kuifunga Man United mara 5 mfululizo.
    Baada ya kuwapiga nje ndani Mahasimu wao wengine LIverpool, Man United, chini ya Meneja Louis van Gaal, hivi sasa ni moto na Rooney ameazimia kudumisha hilo.

    Akiongea na MUTV, Kituo cha TV cha Man United, Rooney alisema: "Hii ni Gemu muhimu kwa Manchester United na Manchester City...na kwa Mashabiki na kwangu mimi ni Gemu kubwa ya kuleta kiburi. Ukichezea Man United unataka ushinde Gemu hizi za Dabi!"
    Aliongeza: "Tunataka tuwape Mashabiki wa United kitu cha kufurahia wakienda kazini JUmatatu, tunataka wao ndio wawacharure Mashabiki wa City huko kazini!"KUKUTANA USO KWA USO
    -Manchester United: Ushindi Mechi 59
    -Manchester City: Ushindi Mechi 49
    -Sare: Mechi 50
    -Jumla: Mechi 168

    0 maoni:

    Chapisha Maoni