Wakazi wa Geita Pasaka hii watapata kuwaona live' Wasanii wa Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers- Bukoba
TAMASHA hilo la PASAKA litafanyika Jumapili tarehe 05/04/2015 sikukuu ya Pasaka yenyewe katika ukumbi wa GEDECO, kuanzia saa 9 mchana hadi 2 usiku.
Kiingilio kwa watu wazima ni kununua tu DVD mpya inayoitwa KAPOTIVE
LIVE SHOW kwa Tshs.10,000 tu. DVD hii inacheza pande zote mbili (Two in
One). Watoto Tshs. 3,000 tu.
Karibuni
sana tusherekee Pasaka kwa shangwe tukiwa na kundi zima la KAPOTIVE
Star Singers-Bukoba. Mratibu wa Tamasha hilo Bw. Andrew Kagya
akizungumza na Mwandishi wetu amewataka Wakaazi wa Mji wa Geita kuingia
kwa Wingi katika Ukumbi huo ili kuburudika kwa Nyimbo za Injili na hapo
hapo Mashabiki watajipatia DVD Mpya ya Kikundi hicho chenye makazi yake
Mkoani Kagera.

Baadhi
ya Waimbaji wa Kikundi cha Kapotive Star Singers wakiimba na kucheza
wimbo wa Kihaya ambao ni moja ya Nyimbo zilizopo kwenye DVD hiyo mpya.
0 maoni:
Chapisha Maoni