
Liverpool wameafikiana dili ya kunsaini
Kijana wa Miaka 22 anaecheza kama Straika wa Burnley iliyoporomoka
Daraja kutoka Ligi Kuu England licha ya Klabu hiyo kuigomea ofa ya
Liverpool.
Danny Ings, anaechezea Timu ya Taifa ya
England ya U-21, anamaliza Mkataba wake na Burnley mwishoni mwa Mwezi
huu lakini kutokana na umri wake mdogo Kanuni zinaitaka Liverpool
kuilipa fidia Burnley. Liverpool wanatarajia kulipa fidia ya kati ya Pauni Milioni 5 hadi 6 lakini ikiwa Burnley watagoma basi suala hilo litaenda kwenye Jopo litakaloamua idadi inayofaa.
Wakati Burnley imesema itaendelea maongezi na Liverpool, Vigogo hao wa England wametangaza watamsaini Ings Julai 1 baada ya kukubaliana malupulupu yake binafsi na ikiwa Mchezaji huyo atafuzu upimwaji afya yake.
Msimu
uliopita, ukiwa ni Msimu wakevwa kwanza kucheza Ligi Kuu England, Ings
alipiga Bao 11 katika Mechi 35 alizoichezea Burnley wakati Mastraika
wanaotambulika huko Liverpool, Daniel Sturridge, Rickie Lambert, Mario
Balotelli na Fabio Borini, wakifunga jumla ya Bao 8 tu huku Raheem
Sterling akipiga 7 na Steven Gerrard kufunga 9.
Ings
atakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Liverpool wakati huu baada ya
Wiki iliyopita kumpata Mchezaji Huru kutoka Man City James Milner.
0 maoni:
Chapisha Maoni