.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 20 Oktoba 2015

Tagged Under:

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: KIKOSI CHA WACHEZAJI MTU 20 WA MAN UNITED WAELEKEA MOSCOW! TAYARI KUKWAANA NA CSKA JUMATANO

By: Unknown On: Jumanne, Oktoba 20, 2015
  • Share The Gag

  • KIKOSI cha Wachezaji 20 wa Manchester United Leo hii wamesafiri kwenda Moscow, Urusi ambako Kesho Usiku watacheza Mechi yao ya Kundi B la UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, na CSKA Moscow.Kikosi hicho kimeundwa na Wachezaji 18 ambao ndio walicheza na kuwa Benchi Jumamosi iliyopita huko Goodison Park walipoichapa Everton Bao 3-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
    Wachezaji Wawili walioongezwa ni Kipa Sergio Romero na Antonio Valencia.

    Kwenye Kundi B kila Timu ina Pointi 3 baada ya Mechi 2 na Mechi hizi za 3 ni muhimu katika kufungua njia ya kufuzu kwenda Raundi ya Mtoano ya Timu 16.

    Mechi nyingine kali za UCL ambazo zitachezwa Kesho ni ile ya Jijini Manchester Uwanjani Etihad wakati Man City wakiikaribisha Sevilla ya Spain kwenye Mechi ya Kundi D na huko Jijini Paris Nchini France ipo Mechi ya Kundi A kati ya Paris St Germain na Real Madrid.
    MAN UNITED WACHEZAJI 20 WALIOKWEA NDEGE NI
    De Gea, Romero, Johnstone, Darmian, Smalling, Jones, Rojo, Blind, Carrick, Schweinsteiger, Schneiderlin, Fellaini, Valencia, Pereira, Mata, Herrera, Memphis, Lingard, Rooney, Martial.

    Meneja wa Man United Van Gaal

    Wayne Rooney

    UEFA CHAMPIONS LEAGUE
    MAKUNDI
    Jumanne Oktoba 20
    KUNDI E

    BATE Borislov v Barcelona
    Bayer Leverkusen v AS Roma

    KUNDI F

    Arsenal v Bayern Munich
    Dinamo Zagreb v Olympiakos

    KUNDI G

    Dynamo Kiev v Chelsea
    FC Porto v Maccabi Tel Aviv

    KUNDI H

    Valencia v KAA Gent
    Zenit Saint Petersburg v Lyon

    0 maoni:

    Chapisha Maoni