.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 22 Oktoba 2015

Tagged Under:

Bastian Schweinsteiger kaamua maamuzi haya kwa kampuni ya kichina iliyotengeneza sanamu yake…

By: Unknown On: Alhamisi, Oktoba 22, 2015
  • Share The Gag

  • Kiungo wa kimataifa wa Ujerumani anayeichezea klabu ya Manchester United ya Uingereza Bastian Schweinsteiger October 22 ameingia katika headlines baada ya mtengenezaji wa midoli wa kichina kutengeneza mdoili unaofanana na yeye na kuita jina lake.
    Bastian-Schweinsteiger-lookalike-Nazi-doll-named-Bastian
    Mdoli huyo ambaye ametengenezwa kwa muonekano wa sura ya Bastian Schweinsteiger na mtengenezaji wa mdoli huyo amempa jina la ‘Bastian’ sawa na jina halisi la kiungo huyo wa Man United, kingine cha jamaa wa kichina aliyetengeneza sanamu hiyo kaiweka katika mavazi ya jeshi la Nazi.
    Bastian-Schweinsteiger-lookalike-Nazi-doll-named-Bastian (1)
    Hata hivyo kiungo huyo aliyeisaidia Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil tayari amewasiliana na mwanasheria wake na wapo katika mpango wa kuishitaki kampuni iliyotengeneza mdoli huo, licha ya kuwa kampuni hiyo imekana kutengeneza mdoli huyo kwa kumfananisha na kiungo huyo na kwa upande wa jina wanasema ‘Bastian’ ni jina ambalo linatumika sana Ujerumani na hawajamlenga Bastian Schweinsteiger.
    Bastian-Schweinsteiger-lookalike-Nazi-doll-named-Bastian (2)

    0 maoni:

    Chapisha Maoni