.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 23 Oktoba 2015

Tagged Under:

DABI YA MANCHESTER: JUMAPILI REFA NI CLATTENBURG, MANCHESTER UNITED v MANCHESTER CITY! NANI KUIBUKA KIDEDEA?

By: Unknown On: Ijumaa, Oktoba 23, 2015
  • Share The Gag

  • REFA Mark Clattenburg ndie atasimamia Dabi ya Jiji la Manchester Jumapili Oktoba 25 Uwanjani Old Trafford wakati Manchester United wakiwavaa Manchester City.
    Clattenburg, mwenye Miaka 40, ndie aliesimamia Dabi iliyopita Uwanjani Old Trafford wakati Man United, chini ya Meneja Louis van Gaal, ilipoinyuka City Bao 4-2 Mwezi Aprili kwa Bao za Ashley Young, Marouane Fellaini, Juan Mata na Chris Smalling

    Msimu huu, Clattenburg ameshachezesha Mechi 2 za City, ambazo waliifunga Watford na nyingine kufungwa na Tottenham, na Mechi 1 ya Man United waliyoifunga Southampton 3-2.
    Kwa Msimu huu, Refa huyo ameshachezesha Gemu 11 na kutoa Kadi za Njano 11 na Kadi Nyekundu 2.


    WIKIENDI hii Ligi Kuu England ina Mechi kali ikiwamo Dabi ya Jiji la La Manchester wakati Manchester United wakiwa Nyumbani Old Trafford kuikaribisha Manchester Cityhapo Jumapili.
    Lakini Jumamosi, Arsenal, ambao wako Nafasi ya Pili kwenye Ligi Kuu England wakiwa na Pointi 19 sawa na Man United na Pointi 2 nyuma ya Vinara Man City, wana nafasi ya kutwaa uongozi ikiwa watashinda Nyumbani kwao Emirates wakicheza na Everton.
    Timu zote hizi za kileleni, City, Arsenal na Man United, zimetoka kwenye Mechi za Kati-Wiki za UEFA CHAMPIONS LIGI za Makundi yao.
    Akiongelea Dabi yao, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amesema ushindi dhidi ya City ni muhimu ili kusisitiza azma yao ya kuwemo kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa Msimu huu.
    Nao Arsenal wanatoka kwenye wimbi zuri la ushindi baada ya kuzichapa Man United na Watford 3-0 kila mmoja kwenye Mechi za Ligi na kisha Juzi kuifunga Bayern Munich 2-0 kwenye Mechi yao ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI.
    Ikiwa Arsenal wataifunga Everton watakaa kileleni mwa Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza kwa karibu Miaka Miwili na kubakia hapo hadi Jumapili ambapo Dabi ya Manchester itaamua kama watabaki huko juu au wataporomoshwa.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni