.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 19 Oktoba 2015

Tagged Under:

KAMATI ZAIDI ZAUNDWA KUISAIDIA TAIFA STARS, SALEHJEMBE, EDO KUMWEMBE, KITENGE WAPEWA KAZI YA KUHAMASISHA

By: Unknown On: Jumatatu, Oktoba 19, 2015
  • Share The Gag

  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA STARS, FAROUKH BAGHOZA AKIMSIKILIZA KATIBU WAKE, TEDDY MAPUNDA.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa Stars iliyoteuliwa hivi karibuni na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bwana Farough Baghozah leo hii amekutana na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kuitambulisha rasmi kamati hiyo.

    Katika kamati hiyo ya Taifa ya Stars wapo Michael Wambura – Makamu Mwenyekiti, Bi Teddy Mapunda – Katibu, Wakili Imani Madega – Mweka Hazina, na wajumbe wengine ni Juma Pinto, Isaac Chanji, Salum Abdalla na Moses Katabaro.
    Pia Mwenyekiti amechukua fursa hiyo kutangaza kamati ndogondogo na wajumbe wake kama ifuatavyo:
     1. Maandalizi ya timu, zikiwemo huduma kwa timu ya Taifa stars
     Mwenyekiti – Imani Madega
     Wajumbe – Msafiri Mgoyi,Teddy Mapunda.
    SALEH ALLY NA EDO KUMWEMBE
    2. Uhamasishaji wa mchezo (Michezo ijayo) na Masoko
     Mwenyekiti – Juma Pinto
     Wajumbe – Baraka Kizuguto, Mlamu Ng’ambi, Charles Hamka, Hashim  Lundenga, Maulid Kitenge, Shaffih Dauda, Salehe Ally, Peter Simon,  Edo Kumwembe na Mahmoud Zubeiry.
     
    3. Kamati ya Fedha
    Mwenyekiti – Farough Baghozah
    Wajumbe – Teddy Mapunda, Michael Wambura, Imani Madega,          Juma Pinto,        Isaac Chanji, Moses Katabaro na Edgar Masoud.
    4. Mikakati ya ushindi – itakuwa na kamati ndogondogo na zitakuwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti Farough Baghozah, Teddy Mapunda, Mohamed Nassoro, Philemon Ntahilaja, Isaac Kasanga, Cresencius Magori.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni