Tagged Under:
HAZARD KWENDA REAL: MOURINHO AMJIA JUU KOCHA WA BELGIUM! SWALI LIKABAKI KUWA JE LEO ATACHEZA?
By:
Unknown
On: Jumamosi, Oktoba 24, 2015
Jose Mourinho amemponda Marc Wilmots kuhusu madai yake kwamba Eden Hazard ataondoka Chelsea na kuhamia Real Madrid
Msimu uliopita Hazard, ambae ni Mchezaji
wa Kimataifa wa Belgium, alitunukiwa Tuzo ya PFA pamoja na ile ya
Wanahabari ya kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka huko England lakini Msimu huu
uchezaji wake umeporomoka.
Wiki iliyopita Mourinho alimpiga Benchi
Hazard wakati Chelsea inaifunga Aston Villa 2-0 kwenye Ligi kwa madai
kuwa anataka kuzuia Timu yake isiruhusu Mabao.
Magazeti kadhaa huko
England yalimnukuu Marc Wilmots, ambae ni Kocha wa Timu ya Taifa ya
Belgium, akisema Hazard, mwenye Miaka 24, anapaswa kuhamia Real Madrid
ilia pate uhuru zaidi wa kucheza na pia kukwepa sulubu nzito ya Soka la
England.
Maneno hayo yamemkasirisha Mourinho ambae amesema: "Kocha
wa Timu ya Taifa ni wa Taifa. Hazard akiwa Timu ya Taifa mimi sisemi
lolote. Lakini Watu wengine hawana maadili na wanazungumzia Wachezaji
wakiwa Klabuni kwao!”
Alipoulizwa
kama Hazard atacheza hii Leo dhidi ya West Ham, Mourinho alijibu:
“Sijui. Kuna Watu wengi wanatoa maoni yao kuhusu uchezaji wa Hazard
Msimu huu. Mimi sipendi kuzungumzia Mtu binafsi.”
0 maoni:
Chapisha Maoni