.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 19 Oktoba 2015

Tagged Under:

RATIBA - UEFA CHAMPIONS LEAGUE:

By: Unknown On: Jumatatu, Oktoba 19, 2015
  • Share The Gag

  • Arsenal hawana njia yoyote ila kuwashambulia Bayern Munich Uwanjani Emirates Jumanne Usiku kwenye Mechi ya Kundi F la UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, kwa mujibu wa Meneja wao Arsene Wenger.
    Arsenal wamechapwa Mechi zao zote mbili za Kundi F kutoka kwa Dinamo Zagreb na Olympiakos na wapo mkiani mwa Kundi hilo na Mechi zao 2 zinazofuata ni dhidi ya Mabingwa wa Germany Bayern Munich.Ikiwa Arsenal watafungwa na Bayern basi wapo hatarini ya kutofuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL kwa mara ya kwanza katika Miaka 16.
    Hii si Mechi rahisi kwa Arsenal kwani Bayern watatinga Jijini London Uwanjani Emirates wakiwa na wimbi la ushindi la Mechi 12 mfululizo.

    Lakini hilo halimtishi Wenger ambae amesema: “Sasa tupo katika hali nzuri na mkazo kwetu ni Mechi hii ya Jumanne.”
    Arsenal hivi sasa wapo kwenye wimbi zuri la ushindi kwenye Ligi Kuu England ambalo limewapaisha hadi Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Vinara Man City.

    Mara ya mwisho kwa Arsenal na Bayern kukutana kwenye UCL ni Mwaka Jana walipotoka 1-1 huko Allianz Arena Jijini Munich na Bayern kushinda 2-0 Uwanjani Emirates katika Mechi yao ya kwanza.
    UEFA CHAMPIONS LEAGUE
    MAKUNDI
    Jumanne Oktoba 20
    KUNDI E

    BATE Borislov v Barcelona
    Bayer Leverkusen v AS Roma

    KUNDI F
    Arsenal v Bayern Munich
    Dinamo Zagreb v Olympiakos

    KUNDI G
    Dynamo Kiev v Chelsea
    FC Porto v Maccabi Tel Aviv

    KUNDI H
    Valencia v KAA Gent
    Zenit Saint Petersburg v Lyon

    Jumatano Oktoba 21
    KUNDI A

    Malmö FF v Shakhtar Donetsk
    Paris St Germaine v Real Madrid

    KUNDI B

    CSKA v Man United
    VfL Wolfsburg v PSV

    KUNDI C

    Atletico Madrid v FC Astana
    Galatasaray v Benfica

    KUNDI D

    Juventus v Borussia Mönchengladbach 

    Man City v Sevilla

    0 maoni:

    Chapisha Maoni