.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 19 Oktoba 2015

Tagged Under:

MAJIMAJI SELEBUKA YATOA TUZO KWA SALEHJEMBE, GAZETI LA CHAMPIONI

By: Unknown On: Jumatatu, Oktoba 19, 2015
  • Share The Gag

  • Mwandishi wa Gazeti la Championi, Nicodemus Jonas wa pili kulia akiwa na vyeti alivyochukuwa kwa niaba ya Blog ya Salehjembe na Kampuni ya Global Publishers vilivyotolewa na Asasi ya Somi katika Tamasha la Majimaji Selebuka. Kulia ni Mkurugenzi Mwenza wa Asasi ya Somi, Prof. Julian Murchison, Dk Damas Ndumbaro- mkurugenzi mwenza wa Somi na Mkuu wa Jumba la Makumbusho mjini Songea, Balthazar Namusya.
    Katika kule kilichoonekana Blogu ya Saleh Jembe ndiyo blog pendwa kwa michezo nchini, imetunukiwa cheti na Asasi ya Songea –Mississippi (Somi) kwa kutambua mchango wake katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2015, lililohitimishwa juzi Jumamosi.

    Tamasha hilo lililenga kudumisha uhusiano wa Jimbo la Songea na Mississippi ya nchini Marekani kiuchumi kwa kuwaninua wajasiriamali pamoja na kudumisha sekta ya michezo mkoani Ruvuma.
    Akizungumza wakati wa kufunga tamasha hilo, kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini Songea, Mkurugenzi Mwenza wa Somi, wakili Dk Damas Ndumbaro alisema: “Saleh Jembe blog ilikuwa bega kwa bega nasi, mwanzo mpaka mwisho wa tamasha hilo.
    “Tunashukuru watu wengi wamehamasika na wamekuwa wakitufuatilia kupitia blogu hii, hivyo ni lazima tulipe fadhaira kwake.”
    Tovuti na Global Pulishers, nayo ilitunukiwa cheti kama hicho kwa sapoti ya kuripoti matukio yote yaliyojili kwenye tamasha hilo, ambayo ni: Riadha, maonyesho ya ngoma za asili, maonyesho ya wajasiriamali, mbio za baiskeli pamoja na utalii wa ndani.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni