.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 31 Oktoba 2015

Tagged Under:

THEO WALCOTT NA ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN KUZIKOSA BAYERN MUNICH NA SPURS!

By: Unknown On: Jumamosi, Oktoba 31, 2015
  • Share The Gag

  • Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain watazikosa Mechi kadhaa za Arsenal kama ilivyothibitishwa na Meneja wa Klabu hiyo Arsene Wenger.
    Wachezaji hao Wawili waliumia Jumanne iliyopita kwenye Mechi ya Raundi ya 4 ya Capital One waliyofungwa 3-0 na Sheffield Wednesday.
    Oxlade-Chamberlain aliumia Dakika ya 5 tu ya Mechi hiyo alipopata tatizo la Musuli za Pajani na kubadilishwa na Walcott ambae nae ilibidi atolewe Dakika ya 19 baada kuumia Musuli za Mguuni.
    Ingawa bado haijathibitika watakuwa nje kwa muda gani, Wenger amethibitisha Wawili hao kuikosa Mechi ya Ligi Kuu England ya Jumamosi Ugenini na Swansea City na pia ile ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI huko Munich watakaporudiana na Bayern Munich.

    Mechi nyingine ambayo Wachezaji hao wataikosa ni ile Dabi ya London ya Kaskazini na Mahasimu Tottenham.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni