Tagged Under:
LUGHA IMEMPOZA KOCHA WA CHELSEA JOSE MOURINHO!
By:
Unknown
On: Jumanne, Oktoba 20, 2015
Kocha
wa Chelsea, Jose Mourinho, amejitetea kuwa kinachodhaniwa ni lugha
mbovu aliyotumia baada ya kushindwa na Southampton ni kwa kuwa
Kiingereza si lugha yake ya mama.
Mourinho alifungiwa mechi moja na
kupigwa faini ya Pauni za Uingereza 50,000 na shirikisho la Kandanda la
Uingereza. Alidai kuwa maafisa wa kandanda nchini humo wanaogopa kuipa
timu yake penalti inayostahili. Madai ya Morinho yalitolewa baada ya
tume huru maalimu kutoa sababu za adhabu hiyo kutolewa na FA. Kocha huyo
machachari wa Chelsea hakuhudhuria kilichomwadhibu lakini alituma
taarifa ya maandishi kujitetea.
Alikiri
kuwa alikosa adabu lakini akakanusha kuwa alitilia shaka hadhi ya refa
Robert Madley. Huku akijitetea, Moorinho alisema kuwa makosa yaliyompata
ni sawa na yale yaliyowahusu makocha wengine watano wa Premier League.
Mbali na kukosoa kiwango cha faini aliyotozwa, Mourinho pia alisema kuwa
kupigwa marufuku uwanjani kwa mechi moja, ambako kumeahirishwa
kutekelezwa kwa mwaka mmoja, "kulimshangaza". Wenger hakuchukuliwa hatua
yo yote alipomsukuma Mourinho katika eneo la wakufunzi katika Stamford
Bridge Oktoba mwaka 2014.
0 maoni:
Chapisha Maoni