.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumapili, 11 Oktoba 2015

Tagged Under:

KOMBE LA DUNIA 2018: LEO TANZANIA UWANJANI MALAWI HUKO BLANTYRE? KUTETEA USHINDI WAO!

By: Unknown On: Jumapili, Oktoba 11, 2015
  • Share The Gag

  • Timu ya Taifa ya Tanzania Leo hii inajitupa Uwanja wa Kamuzu Banda huko Blantyre kurudiana na Wenyeji Malawi katika Raundi ya Kwanza ya Kanda ya Afrika ya Mchujo wa Kombe la Dunia ambazo Fainali zake zitafanyika huko Russia Mwaka 2018.
    Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Jumatano iliyopita Tanzania iliichapa Malawi 2-0 kwa Bao za Maprofeshanali Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wote hucheza huko Congo DR kwenye Klabu ya Lubumbashi TP Mazembe.
    Kikosi cha Tanzania huko Malawi kipo chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa.
    Ikiwa Tanzania watafanikiwa kuvuka kigingi hiki cha Malawi basi kwenye Raundi ya Pili watavaana na Algeria ambao wanaanzia hatua hiyo.
    Washindi wa Raundi ya Pili wataingizwa kwenye Droo ya kupanga Makundi 5 ya Timu 4 kila mmoja ambapo Washindi wake wataenda Fainali Russia moja kwa moja.



    KOMBE LA DUNIA 2018
    RATIBA:
    Afrika-Raundi ya Awali- Marudiano
    Jumapili Oktoba 11

    15:00 Malawi v Tanzania [0-2]
    16:00 Ethiopia v Sao Tome And Principe [0-1]
    16:00 Kenya v Mauritius [5-2]

    Jumanne Oktoba 13
    14:30 Madagascar v Central African Republic [3-0]
    16:00 Burundi v Seychelles [1-0]
    17:00 Sierra Leone v Chad [0-1]
    18:00 Namibia v Gambia [1-1]
    18:00 Niger v Somalia [2-0]
    19:00 Lesotho v Comoros [0-0]
    19:00 Guinea-Bissau v Liberia [1-1]
    20:00 Botswana v Eritrea [2-0]
    20:00 Swaziland v Djibouti [6-0]
    20:00 Mauritania v South Sudan [1-1]

    0 maoni:

    Chapisha Maoni