.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatano, 9 Septemba 2015

Tagged Under:

Diamond katajwa tena kwenye tuzo nyingine kimataifa… pembeni Davido, Yemi Alade & AKA!

By: Unknown On: Jumatano, Septemba 09, 2015
  • Share The Gag

  • Msanii wa Bongo Flava Diamond Platnumz anazidi kuipeperusha bendera ya Tanzania, Tuzo nyingi sana zinazidi kutambua juhudi na kazi ya Diamond  kwenye muziki wa Tanzania.
    Good news kwako mtu wangu, mtu wetu Diamond Platnumz amepata nafasi nyingine kubwa ya kuiwakilisha Tanzania kwenye tuzo za kimataifa.
    mtvema
    Tuzo za MTV Europe Awards maarufu kama MTV EMA kwa mwaka huu wa 2015 zimemtaja Diamond Platnumz kuwa miongoni mwa wasanii kutoka Africa wanaowania kipengele cha ‘Best African Act’,  wasanii wengine waliobahatika kuingia kwenye kipengele hicho ni; Davido, AKA (South Africa) na Yemi Alade (Nigeria).
    yemimtv
    Yemi Alade ni msanii pekee wa kike kwenye kipengele hiki cha Best African Act.
    davidoema
    Davido kutoka Nigeria
    akaema
    AKA kutoka South Africa.
    MTV EMA 2015 inahitaji mtu wa tano kukamilisha orodha ya ‘Best African Act’ mtu wangu na kama wewe ni mdau mkubwa sana wa muziki mzuri basi MTV EMA 2015 inakupa wewe nguvu na kibali cha kumchagua mtu wa 5 unaehisi atafaa kuchuana na Diamond Platnumza na wengine kwenye kipengele hiki..
    ema2
    kwenye wale watano waliopendekezwa wapo; Wizkid, KO (South Africa), Stone Bwoy (Nigeria), Cassper na DJ Arafat.
    EMA
    Kumpata mmoja kati ya watano hapo juu, utaratibu wa kuwapigia kura upo hivi… unaandika #MTVEMA ikifuatiwa na hashtag (#Nominate) na jina la msanii na kisha unatweet mara nyingi uwezavyo kwenye Twitter ili kumpata yule unayeona anastahili kufunga kipengele hiki.
    EMA1
    Tuzo za MTV EMA Awards 2015 zinafanyika tarehe 25 October jijini Milan, Italy. Mwisho wa kupiga kura ni tarehe 14 September 2015.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni