BEKI
 wa kimataifa wa Senegal, Papy Djilobodji amesaini Mkataba wa miaka 
minne kujiunga na Chelsea kutoka Nantes ya Ufaransa kwa ada ya Pauni 
Milioni 3.
Mabingwa
 wa Ligi Kuu ya England, wamemsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 
27 baada ya mpango wao wa kumcbhukua beki wa Everton, John Stones 
kushindikana tena.
Chelsea
 imeruhusu mabao tisa kutinga nyavuni mwake katika mechi nne na kupoteza
 pointi nne hivyo kujikuta wanazidiwa pointi nane na vinara Manchester 
City. 
Beki wa Senegal, Papy Djilobodji amesaini Mkataba wa miaka minne kujiunga na Chelsea kutoka Nantes  
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

 
0 maoni:
Chapisha Maoni