Wachezaji wa Argentina wakipongezana baada ya kuifunga bao 6-1 Paraguay
Ndani ya Estadio Municipal Alcaldesa Ester Roa Mjini Rebolledo
Nchini Chile, Argentina wameitandika Paraguay katika Nusu Fainali ya
Pili ya Copa America. BAO za Argentina zimefungwa na Marcos Rojo 15'
Javier Pastore 27'
Ángel Di María 47'
Ángel Di María 53
Bao la Paraguay limefungwa na Lucas Barrios dakika ya 43 kipindi cha kwanza.Ushindi wa Argentina asubuhi hii kuifanya kwenda nusu Fainali na kukutana uso kwa uso na Wenyeji Chile ambao wametinga Fainali baada ya kuichapa Peru 2-1.
Lionel MessiBaada ya kukutana awali katika Mashindano haya na kutoka Sare 2-2 katika Mechi ya Kundi lao ambayo Argentina waliongoza Bao 2-0 kabla Haftaimu na Paraguay kusawazisha, safari hii pia Argentina waliongoza 2-0 kwa Bao za Marcos Rojo na Pastore, zilizotengenezwa na Nahodha wao Lionel Messi.
0 maoni:
Chapisha Maoni