.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 13 Machi 2015

Tagged Under:

DAVID LUIZ AOMBA RADHI BAADA YA KUIFUNGA TIMU YAKE YA ZAMANI CHELSEA.

By: Unknown On: Ijumaa, Machi 13, 2015
  • Share The Gag

  • BEKI wa Paris Saint-Germain, David Luiz amewaomba radhi Chelsea baada ya kushangilia bao alilofunga ambalo lilisaidia kuing’oa timu yake hiyo ya zamani katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Luiz alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 86 ya mchezo huo na kusababisha mchezo huo kwenda katika muda wa nyongeza. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 amesema anaomba radhi kwa kuonyesha hisia zake kwani ilikuwa vigumu kujizuia kutokana na furaha aliyokuwa nayo. PSG ilisonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa faida ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo huo. Luiz amewahi kuichezea Chelsea mechi 143 katika mashindano yote na kufunga mabao 12 kabla ya kuhamia PSG kwa kitita cha paundi milioni 40 Juni mwaka jana.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni